![]() |
Mji wa Runzewe ni mji ambao upo katika mkoa Mpya wa Geita. Ni mji ambao wananchi walikuwa hawafikirii kama serikali itawakumbuka katika suala zima la kuwaletea umeme, ila kwa sasa wameziona dalili za umeme kwamba utawaka.Shebby D aliongea na baadhi na wananchi wanasemaje kuhusiana na hili suala la umeme wengi wao walionekana ni watu yenye furaha sana, kiufupi tatizo la umeme kwao limekuwa ni kubwa sana, na kwa sasa gharama wanazotumia kwenye umeme ni kubwa sana ukilinganisha na mazingira ya miji ambayo ina umeme wa Tanesco. Inasemekana kwa sasa mtu mwenye kibanda cha kuchaji simu au mwenye friji wanalipia sh 4000/- hadi 5000/- kwa siku ambapo kwa miji yenye umeme wa Tanesco bili hiyo wanalipa kwa mwezi, vilevile hata wanaotumia umeme majumbani kwao imekuwa ni shida tupu unakuta umeme unasumbua lakini akija mwenye mashine ya umeme anataka sh 40000/- hadi sh 60000/- kwa mwezi.
Wameiomba serikali ifanye jitihada za kuleta umeme kwani wamechoka kutaabika na umeme wanaotumia sasa.Katika mkutano uliofanyika hivi karibuni Mbunge wa jimbo la Bukombe Pro Kahigi alitoa ahadi kuwa ifikapo mwezi wa 11 (november) mwaka huu umeme utakuwa umewaka.Swali kubwa ambalo wanajiuliza baadhi ya wananchi je kweli umeme utawaka kama walivyo ahidi au mpaka kampeni zifike?

Kuna sehem nyingi sana tu bado hatujapata umeme kwahyo kama uwezekano upo wa sehem zotekuwa na umeme kuambiwe kwan biashara zetu znakwama
JibuFuta