TANGAZO

TANGAZO

Jumatatu, 25 Agosti 2014

Huu ndo mchakato wa umeme Runzewe.....


Mji wa Runzewe ni mji ambao upo katika mkoa Mpya wa Geita. Ni mji ambao wananchi walikuwa hawafikirii kama serikali itawakumbuka katika suala zima la kuwaletea umeme, ila kwa sasa wameziona dalili za umeme kwamba utawaka.Shebby D aliongea na baadhi na wananchi wanasemaje kuhusiana na hili suala la umeme wengi wao walionekana ni watu yenye furaha sana, kiufupi tatizo la umeme kwao limekuwa ni kubwa sana, na kwa sasa gharama wanazotumia kwenye umeme ni kubwa sana ukilinganisha na mazingira ya miji ambayo ina umeme wa Tanesco. Inasemekana kwa sasa mtu mwenye kibanda cha kuchaji simu au mwenye friji wanalipia sh 4000/- hadi 5000/- kwa siku ambapo kwa miji yenye umeme wa Tanesco bili hiyo wanalipa kwa mwezi, vilevile hata wanaotumia umeme majumbani  kwao imekuwa ni shida tupu unakuta umeme unasumbua lakini akija mwenye mashine ya umeme anataka sh 40000/- hadi sh 60000/- kwa mwezi.  
 Wameiomba serikali ifanye jitihada za kuleta umeme kwani wamechoka kutaabika na umeme wanaotumia sasa.Katika mkutano uliofanyika hivi karibuni Mbunge wa jimbo la Bukombe Pro Kahigi alitoa ahadi kuwa ifikapo mwezi wa 11 (november) mwaka huu  umeme utakuwa umewaka.Swali  kubwa ambalo wanajiuliza baadhi ya wananchi je kweli umeme utawaka  kama walivyo ahidi au mpaka kampeni zifike?

Huu hapa ndo mjengo mpya anaoujenga kisura wetu kutoka pande za Runzuwe Tamali (SADA) ni waukweri ucheki hapa

Hakika ukijituma sana na mafanikio utayaona na moja ya mafanikio hayo ni pamoja na ujenzi. Haya hapa ni baadhi ya mafanikio aliyopata aliyopata kisura wetu kutoka pande za Runzewe.   Shebby D Blog inampa ongera sana akomae hivyo hivyo . Msome bofya hapa   na kupitia facebook huyu hapa

Jumamosi, 27 Julai 2013

NANI WA KULAUMIWA KWA HALI YA SASA YA RUNZEWE?


Na mwandishi wetu.
Conrad
Kwa miongo kadhaa sasa mji wetu ume kuwa ukitegemea kipato kutokana na shughuli za uchuuzi wa madini ya dhahabu kutoka kwa vijana almaarufu kama NGONI japo hamna alitokea RUVUMA-Songea. wanako ishi watu kabila la Wangoni.
Kiuhalisia kwa sasa hali ya utendaji na uingizaji wa Shilingi hapa mtaani kwetu ime kuwa ngumi tena Ngumu sana baada ya NGONI hao kupigwa marufuku na kuwekewa ulinzi mkali huko POLI. Yaani kiufupi mzunguko wa hela umepwaya sana. Hela ilizunguka kwa Mfumo kama huu
Bodaboda
Ngoni
Wenye baa na wauzaji wa mvinyoo wengine

Wenye Nyumba za Wageni.
Mama Ntilie
Wauzaji wa maji.
kwa utaratibu huu RUNZEWE yetu ilikuwa na hekaheka za kila mtu

kutafuta fedha ambayo ilikuwa inapatikana hapa kwetu.
baada ya kuwazuia Ngoni runzewe ime poa hadi kufukia watu na wakaazi wengine kuamua kuhama. Yaani wamefunga bidhaaa na shughuli zao walizo kuwa wakifanya awali.
Jamani wanaRunzewe tufanye nini kurudia hali yetu ya awali kukidhi kuyamudu maisha yetu ya kila siku?
je, tuwavamie walinzi wa mgodi? jibu ni hapana kwani italeta maafa
je, tuandamane hadi wizara ya KAZI na AJIRA? itachukua muda kupata sitahiki zetu.
basi ni muda sasa wa kutafuta vyanzo mbadala vya mapato hapa mtaani kwetu.
vyanzo hivyo ni kama....
Uchuuzi wa mazao
Uoteshaji wa miche ya miti na maua.
na nyingine nyingi kama zilivyo aniinishwa na wizara ya Kazi na Ajira